Umuhimu wa Tovuti kwenye biashara yako

Je unahitaji kuwa na tovuti kwa ajili ya biashara?

Hilo ni swali kila mtu mwenye biashara hujiuliza. Wengi tumekuwa hatujui umuhimu wa tovuti. Labda kwasababu majibu tuliokua nayo ni “gharama sana”, “inahitaji mda”, “teknolojia ngumu”, “nina biashara kubwa ya kutosha sihitaji moja”. Yote hayo yanaweza kukufanya usione umihumu wa kuwa na tovuti.

 

Sasa je bado unajiuliza haja ya biashara yako kuwa na tovuti?

Kabla sijakupa mchanganuo wa umuhimu wa tovuti kwa ajili ya biashara yako nahitaji utambue kuwa asilimia zaidi ya 80% ya watu wenye uwezo ya kuingia kwenye mtandoa hufanya utafiti wa biashara mtandaoni

1. Tovuti itafanya biashara yako iaminike zaidi

Je unafahamu ni vitu gani huleta uaminifu kwenye biashara. Ukiachana na mahali au eneo la biashara. Tovuti yako itajenga uaminifu kwa kusema, mimi niko hapa, ninamaanisha biashara, na niko kwa muda mrefu.
Kwa kupanga kwa uangalifu, kwa busara na kwa kuangalia mahitaji ya wateja wako, wavuti yako itatoa picha ya kitaalam na kuwapa wateja uwezo mkubwa wanapotembelea, iwe iko kwenye kompyuta zao, tableti au simu.

2. Huhifadhi Muda.

Muda ni pesa, kwa hiyo mara nyingi huunganishwa pamoja. Kuwasiliana na kutimiza haja wateja huchukua muda. Wavuti yako inaweza kuokoa muda huo kwa kutoa majibu ya maswali na maoni ya kawaida kwa wateja bila ya kurudia ujumbe huo huo kwa watu tofauti.
Unaweza kutumia wakati wako kufanya vitu vya thamani zaidi, kama kuendeleza biashara yako.

3. Hurahisisha upatikanaji wa Biashara yako.

Kuwa na tovuti hufanya iwe rahisi sana kwa watu kukupata, kusoma juu ya biashara yako, unachofanya na kujibu rundo la maswali waliyo nayo kwa ajili ya biashara yako. Kwa kuwa na tovuti watu wataweza kupata biashara yako wanapoitafuta kwenye injini za utaftaji kama google, yahoo au bing. Wakati mwingine mtu asipofanikisha kupata biashara yako mtandaoni anaweza akahis biashara yako imefungwa.

4. Fursa za kimataifa

Ukiwa na tovuti hufanya uwezekano kwa mtu yeyote ulimwenguni kupata biashara yako. Ikiwa unayo bidhaa/huduma ambayo inaweza kuuzwa kwa urahisi mtandaoni unaweza kuongeza kiwango kikubwa cha wateja wako kwa kuuza kwenye mtandao.

Au labda huwezi kuuza huduma/bidhaa zako mkondoni lakini kwa kuwa na wavuti unaweza kupata wateja ambao wako nje ya mahala pako kijiografia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *